Breaking

Thursday 17 March 2022

MAGAIDI WASHAMBULIA BASI NA KUUA WATU 21 - NIGER



Magaidi wenye silaha wameshambulia basi na lori moja na kuua watu wasiopungua 21 katika eneo la kusini magharibi mwa Niger, karibu na mpaka wa nchi hiyiio na Burkina Faso.

Duru za kieneo za Niger zimethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, shambulio hilo limetokea jana Jumatano Machi 16, 2022 karibu na mpaka wa Burkina Faso ambalo umekuwa uwanja wa vitendo kama hivyo vya kigaidi tangu mwaka 2015.

Mbali na kuuawa watu 21 katika shambulio hilo lililotokea katika eneo la Tillabéri, magaidi hao wenye silaha limejeruhi watu wengine wengi.

Maafisa wa eneo hilo wametoa ufafanuzi kwa kusema, wasafiri 19 wakiwemo maafisa wawili wa polisi ndio waliouawa huku Watu wengine wawili waliokuwemo kwenye lori nao wameuliwa na magaidi hao na kufanya idadi ya waliouawa kufikia watu 21.


Siku chache zilizopita, watu wasiopungua 11 waliuawa katika shambulizi la watu wenye silaha kwenye mgodi mmoja wa dhahabu, kaskazini mwa Burkina Faso.


Shambulio hilo lilitokea siku mbili tu baada ya shambulizi jingine kama hilo kwenye sehemu hiyo hiyo.

Mkazi mmoja wa eneo hilo akiliambia shirika la habari la AFP kwamba watu wasiojulikana wenye silaha wamefanya shambulio hilo kwenye mgodi wa madini ya dhahabu katika eneo la Baliata.

Alhamisi wiki iliyopita pia watu 14 waliuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia mgodi wa dhahabu katika mji Seytenga wa jimbo la Séno la kaskazini mwa Burkina Faso.


Nchi za magharibi mwa Afrika za Mali, Niger na Burkina Faso zimekumbwa na mashambulizi ya mfululizo ya magaidi wakufurishaji kama ilivyo kwa Nigeria.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages