Breaking

Sunday 6 March 2022

MAGAIDI WAUA WANAJESHI 27 - MALI




Magenge yenye silaha yameshambulia kambi ya kijeshi katikati ya Mali jana Ijumaa na kuua wanajeshi 27 serikali.

Jeshi la Mali limethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, magaidi 47 wameangamizwa kwenye shambulio hilo.

Mapigano hayo yamepelekea wanajeshi 33 wa serikali kujeruhiwa, 21 wamejeruhiwa vibaya wanajeshi saba hadi hivi sasa hawajulikani. Jeshi la serikali limesema kuwa, magaidi 23 waliangamizwa siku moja baadaye.

Nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika imekuwa ikipambana na magenge ya kigaidi huku karibu thuluthi mbili ya ardhi ya nchi hiyo ikiwa nje ya udhibiti wa serikali.

Afisa mmoja wa jeshi la Ufaransa ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema, mamia ya magaidi walishambulia kambi iliyokuwa na wanajeshi takriban 150 wa serikali, na kuua baina ya wanajeshi 40 hadi 50.



Afisa huyo wa jeshi la mkoloni Mfaransa pia amesema, magaidi hao waliteka magari 21 ya kijeshi pamoja na vifaru na kujeruhi zaidi ya wanajeshi 20 wa serikali ya Mali.

Shambulio hilo limetokea kwenye kambi ya kijeshi ya Mondoro iliyoko karibu na mpaka wa Mali na Burkina Faso. Huko nyuma pia magenge yenye silaha yaliwahi kuivamia kambi hiyo kwa madai ya kupambana na wanajeshi wa kigeni.

Shambulio hilo la jana limetokea baada ya serikali ya Mali kumtaka mkoloni Mfaransa kuondoa wanajeshi wake nchini humo ikiishutumu Paris kwa kushirikiana na magenge ya kigaidi kuhatarisha usalama wa kitaifa wa Mali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages