Breaking

Wednesday 9 March 2022

RAIS PUTIN ADAIWA KUISHI TANZANIA KWA MIAKA MINNE



Rais wa Urusi Vladimir Putin 
anayelalamikiwa kwa uvamizi nchini Ukraine, amedaiwa kuwahi kuishi nchini Tanzania kwa miaka minne mfululizo tangu mwaka 1973-1978.

Mtandao wa iHarare wa Nchini Zimbambwe mnamo December 10, 2018 ulichapisha habari na picha ikidaiwa kumuonesha Putin akiwa na baadhi ya wapigania Uhuru wa Afrika wakiwa katika viunga vya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani.



Kwa mujibu wa historia, Bagamoyo ilikuwa mongoni mwa vituo vya kuwahifadhi wapigania Uhuru wa Afrika ambapo Putin anatajwa kuwepo katika kituo hicho kwa ajili ya kuwapatia mafunzo wapiganaji hapo.


Katika picha iliyochapishwa na iHarare, mwandishi ameiwekea maelezo picha hiyo kuwa miongoni mwa wapigania uhuru walioonekana katika picha hiyo ni pamoja na rais wa sasa wa Zimbambwe, Emmerson Munangagwa.

Mwingine aliyetajwa kwenye maelezo hayo ya picha inayodaiwa kupigwa mwaka 1973 ni Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel licha ya ripoti nyingine kudai kuwa picha hiyo imepigwa nchini Ujerumani miaka ya 1980.


Wakati huo ilikuwa ni miaka michache tu tangu Tanganyika kupata Uhuru wake, Desemba 9, 1961 kutoka kwa Uingereza, ndipo Tanganyika ikawa mstari wa mbele kuzisaidia nchi nyingine za Afrika kujikomboa mpaka miaka ya 1980.


Wapigania uhuru wengi wa Msumbiji na Afrika Kusini walifichwa katika maeneo ya Mazimbu Morogoro na Kaole Bagamoyo yote ni maeneo yaliyopo Tanzania (Tanganyika zamani).

Urusi na Tanzania zimetajwa kuwa na uhusiano wa karibu tangu enzi za uongozi wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, kiasi kwamba madaktari wengi wa Tanzania walichukuliwa na kwenda kusoma Moscow, Urusi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages