Breaking

Saturday 12 March 2022

RAIS SAMIA ATAKA KUUNDWA KWA KANUNI ZA MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA


Na Samir Salum - Lango la habari 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.





Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Jumamosi Machi 12, 2022 baada ya kupokea maazimio ya awali kutoka Kikosi kazi alichokiteua cha kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa uliofanyika jjiini Dodoma Desemba 15 hadi 17, 2021.



Rais Samia amemwagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), 
Dkt. Balozi Pindi Chana kushirikiana na Tanganyika Iaw Society (TIS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) kutengeneza kanuni hizo.





Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 24, na ambacho kinawajibika moja kwa moja kwa Rais, kiliwasilisha maazimio hayo Ikulu Jijini Dodoma.


Taarifa imeeleza kuwa Maazimio hayo yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji ambapo azimio la muda mfupi ni la kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.


Aidha imeeleza Baadhi ya maazimio ya muda wa kati ambayo ni pamoja na Rushwa na maadili katika uchaguzi, Ruzuku, Elimu ya uraia, huku masuala yanayohusu Uchaguzi na Katiba mpya vikiwa ni mpango wa muda mrefu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages