Breaking

Friday 25 March 2022

STEVE NYERERE AJIUZULU USEMAJI WA SHIRIKISHO LA MUZIKI





Msanii maarufu wa filamu nchini na mchekeshaji, Steve Mengere maarufu Steve Nyerere, ambaye alikuwa ameteuliwa kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania(SMT), ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.


Steve ametangaza uamuzi huo leo Ijumaa Machi 25, 2022 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya wasanii kudai kuwa hana sifa za kuliongoza Shirikisho hilo.


Amesema sababu za yeye kujiuzulu usemaji ni kuwa hawezi kuongoza watu ambao wana shinikizo, na kwamba kelele zinazoendelea kuhusu yeye hazina tija kwa Taifa.


Ameongeza kuwa anataka kuwa kiongozi ambaye anawaunganisha watu kwa maslahi ya Taifa.


“Nimeamua kuachia ngazi niendelee na kazi zingine za msingi. Nitatoa ushirikiano kwa shirikisho pale nitakapohitajka kushirikiana. Siwezi kuwa kiongozi ninaoongoza watu wenye shinikizo, sifa ya kiongozi haiwi hivyo, nia ilikuwa kutengenza njia. Hizi kelele hazina tija kwenye Taifa letu tuna mambo ya msingi katika kumsapoti Mheshimiwa Rais, siwezi kugombania usemaji,” amesema Steve


Aidha, Steve ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais na shirikisho hilo wakati wote huku akiwasihi wasanii kuendelea kushirikiana na kupendana.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages