Breaking

Monday 7 March 2022

URUSI KUSITISHA MASHAMBULIZI KURUHUSU RAIA KUONDOKA KATIKA MJI MKUU WA UKRAINE KYIV



Na Samir Salum - Lango la habari 

Jeshi la Urusi limesema litasitisha mapigano leo Jumatatu Machi 07, 2022 kuanzia saa 10 asubuhi saa za Moscow katika miji kadhaa ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Kyiv na Mariupol ili kuruhusu Raia kuondoka.

shirika la habari la Interfax liliitaja wizara ya ulinzi ya Urusi kusema kuwa mapigano hayo pia yatasitishwa katika miji ya Kharkiv na Sumy, ikiwa ni ombi la Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Kulingana na ramani zilizochapishwa na shirika la habari la RIA imeonesha kuwa Raia kutoka Kyiv watapitia mpaka wa Belarusi, na raia kutoka Kharkiv watapitia mpaka unaoelekea Urusi.

Pia Raia waliopo katika miji ya Mariupol na Sumy watapitia katika mpaka wa Urusi.

Aidha, Wizara hiyo imeeleza kuwa Wale wanaotaka kuondoka Kyiv pia wataweza kusafirishwa kwa ndege hadi Urusi, ikiongeza kuwa itatumia ndege zisizo na rubani kufuatilia uhamishaji na "majaribio ya upande wa Ukraine kuihadaa Urusi na ulimwengu mzima uliostaarabu ... ni bure. wakati huu".

Tangazo Mwishoni mwa juma Ukraine ilisema mashambulizi ya Urusi katika miji ya mashariki, ikiwa ni pamoja na bandari ya Mariupol, yalikuwa yanawazuia wakaazi kuhama eneo hilo kwenye korido zilizokubaliwa katika duru ya mwisho ya mazungumzo ya kusitisha mapigano.


Social embed from twitter

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages