Na Samir Salum
Raia wataruhusiwa kuondoka katika mji wa Mariupol nchini Ukraine kati ya saa Sita mchana hadi saa 11 jioni (12 : 00-17 : 00 ) kwa saa za Moscow siku ya leo Jumamosi Machi 05, 2022.
Wizara ya ulinzi ya Uruzi imethibitisha hilo na mapema leo Jumamosi na kuongeza kuwa wanajeshi wake ambao wameuzingira mji wa bandari wa Bahari ya Azov kusini mwa Ukraine wataacha kufyatua risasi na kuruhusu raia kupita.
"Kuanzia saa 10 : 00 asubuhi kwa saa za Moscow (07 : 00 GMT), upande wa Urusi unatangaza kusitisha mapigano na kufunguliwa kwa korido za kibinadamu ili kuruhusu raia kuondoka Mariupol na Volnovakha," mashirika ya habari ya Urusi yalinukuu wizara ya ulinzi ya Urusi ikisema.
Mariupol ni mji muhimu wa bandari na imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kutoka Urusi kwa siku kadhaa.
Kumekuwa na mapigano makali Volnovakha
Mapema, meya wa Mariupol alitoa wito wa raia kuruhusiwa kuondoka huku kukiwa na kile alichokiita "kizuwizi" cha vikosi vya Urusi
Mapema, meya wa Mariupol alitoa wito wa raia kuruhusiwa kuondoka huku kukiwa na kile alichokiita "kizuwizi" cha vikosi vya Urusi
Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine leo Jumamosi imesema kuwa zaidi ya wanaume 66,200 wa Ukraine wamerejea kutoka nje ya nchi kupigana.
Kwingineko, mapigano yanaendela. Milipuko mingi ilisikika katika Kharkiv, Kaskazini Mashariki mwa ukraine
Katika mji wa mashariki wa Sumy ambao umezingirwa na vikosi vya Urusi mashambulio ya anga yalianzakumi na moja alfajiri, kulingana na vyombo vya Habari vya Ukraine.