Breaking

Monday 7 March 2022

URUSI YATOA MASHARTI YA KUSITISHA VITA UKRAINE


Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha mashambulizi yake wakati wowote ikiwa Ukraine itatimiza masharti yake.


Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov ameliambia shirika la habari la Reuters leo Jumatatu Machi 07, 2022 kuwa Urusi inaitaka Ukraine ibadili katiba na isitishe hatua ya kutaka kujiunga na upande wowote kama vile NATO.


Amesema kuwa inataka Ukraine itambue Rasi ya Crimea iliyotwaliwa kama eneo la Urusi mikoa ya Donetsk na Luhuansk mashariki mwa Ukraine itambulike kama mataifa huru.


Peskov amambia shirika la habari la Reuters kwamba madai yote yameandaliwa na kutangazwa wakati wa duru mbili za kwanza za mazungumzo kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine, ambayo yalifanyika wiki iliyopita.


Aidha, Ameongeza kuwa Urusi itaondoa jeshi Nchini Ukraine ikiwa masharti haya yatatimizwa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages