Breaking

Wednesday 9 March 2022

WAHAMIAJI HARAMU 78 WAKAMATWA WAKIWEMO WATANZANIA




Jeshi la Uhamiaji Mkoani Iringa kwa kushirikiana na ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) limewakamata wahamiaji haramu 78 raia wa Ethiopia na Watanzania wawili.


Akithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao leo Jumatano Machi 09, 2022 Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji mkoani Iringa SACI Agnes Luziga, amesema raia hao wamekamatwa jana Machi 8, 2022, majira ya saa 1:00 jioni.

Luziga ameeleza kuwa jana jioni alipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna gari linasadikiwa kubeba wahamiaji haramu ambalo katika gari hilo kulikuwa na kulikuwa na stika ya TRA ambayo ilikuwa sio rahisi kugundulika.

Amesema baada ya kukamata gari hilo, walishirikiana na TRA kulikagua gari na kulifungua na kutokana na stika hiyo wahamiaji hao waliingia ndani ya kwa kupitia matundu yaliyokuwa yametobolewa juu ya gari hiyo.

"Wahamiaji tuliowakamata ni raia wa Ethiopia wametokea Ethiopia kupitia mpaka wa Hororo-Taveta wakielekea nchini Afrika Kusini wakienda kutafuta maisha, hivyo taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hawa zinaendelea," amesema Agnes.

Aidha, Kamishna Msaidizi Luziga ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa katika ofisi za uhamiaji pindi wanapoon au kuhisi uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo yao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages