Breaking

Tuesday 8 March 2022

WATU 406 WAUAWA HUKU 800 WAKIJERUHIWA UKRAINE

 

Umoja wa Mataifa umetangaza leo Jumanne Machi 08, 2022 kuwa watu 1,207 wamepata madhara tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuanza tarehe 24 Februari.

Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Liz Throssell,  amesmea kuwa idadi hiyo inajumuisha watu 406 waliouawa na 801 kujeruhiwa japo ameeleza kuwa inaweza kuwa ni zaidi. 

"Majeraha mengi ni matokeo ya mashambulio ya anga na silaha za milipuko namamia ya majengo ya makazi yameharibiwa katika miji kote Ukraine" amesema

Mwanahabari mmoja anaripotiwa kuuawa. Umoja wa Mataifa pia umeelezea wasiwasi wake kuhusu "kukamatwa kiholela" kwa wafuasi wanaounga mkono Ukraine katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa kijeshi wa Urusi - pamoja na ghasia dhidi ya wale wanaochukuliwa kuwa wanaounga mkono Urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Ukraine.

Takwimu za hivi punde za Umoja wa Mataifa zinaonesha takriban watu 12,700 wamekamatwa nchini Urusi kwa kufanya maandamano ya amani ya kupinga vita.

Shirika hilo lilikosoa "sheria kandamizi" zilizowekwa na Urusi hivi karibuni ambazo zinaweka kifungo cha hadi miaka 15 jela kwa wale wanaoshtakiwa kwa kueneza habari iliyoitwa ya "uongo" kuhusu uvamizi huo, au kudharau vikosi vya jeshi la Urusi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages