Na Samir Salum - Lango la habari
Ikiwa ni miaka miwili tangu kuthibitika kwa Mgonjwa wa Uviko - 19 Nchini hadi kufikia Machi 12, 2022 Jumla ya watu 33,789 wamethibitika kuwa na ugonjwa huo huku 803 wakipoteza maisha.
Hayo yameelezwa leo Jumatano Machi 16, 2022 na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa ya miaka miwili ya mwenendo wa ugonjwa wa UVIKO-19 na kutoa pole kwa wahanga wote waliokumbwa na ugonjwa huu.
Waziri Ummy amesema katika kipindi cha miaka miwili mikakati iliyotekelezwa na Serikali ni pamoja na kuwaondoa hofu wananchi ikiwemo kufunga Shule, Vyuo na Taasisi za Elimu ya juu, kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na ugonjwa huu, kusitisha mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kuimarisha huduma za ukaguzi na uchunguzi wa afya kwa wasafiri katika maeneo ya viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu na kuboresha mchango wa tiba asili.
Akielezea hali ya chanjo nchini Waziri Ummy amesema Serikali imeendelea kuikinga jamii kwa kuwezesha upatikanaji wake ambapo jumla ya watu milioni 2.82 wamepata chanjo kamili kati ya watu milioni 30.7 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ikiwa ni sawa na asilimia 9.17.
"Idadi hii bado hairidhishi kwa kuwa ili tuweze kufikia kinga ya jamii (Heard immunity) tunapaswa kuchanja angalau asilimia 70 ya watu wenye umrii wa miaka 18 na kuendelea" amesema Waziri Ummy
Amesema kuwa kutokana na mikakati iliyotekelezwa ikiwemo kuchukua tahadhari na Chanjo hali ya maambukizi katika wimbi la nne nchini imepungua tokea Desemba 2021 ambapo watu 4285 walithibitika na maambukizi, Januari watu 2737 na Februari walikua 401.
"Kupungua huku kumeripotiwa na nchi nyingine duniani na kusababisha kulegezwa kwa masharti ya kujikinga" amesema Waziri Ummy
Amesema ndani ya wiki hii kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa na WHO kuhusu kuibuka kwa kirusi kipya cha UVIKO-19 ktk nchi za China, Korea kusini na Japan hivyo wizara inaendelea kuwasiliana na WHO sambamba na kuimarisha ukaguzi na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia.

Waziri Ummy ameongeza kuwa kutokana na kupungua kwa maambukizi duniani, Serikali imelegeza masharti ya wasafiri wanaoingia nchini kuanzia kesho trh 17/3/2022 ambapo kunaondolewa hitaji la kuwa na cheti cha kipimo (Negative RT-PCR Certificate) kilichokua kikihitajika hapo awali.
Aidha, amewaasa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko-19 (Covid-19) ikiwemo kuvaa barakoa, matumizi ya sanitizer na kuchoma chanjo.
"narudia kusisitiza kuwa UVIKO-19 bado upo na hutokea kwa mtindo wa mawimbi yanayoambatana na mabadiliko mbalimbali. Hivyo kila mmoja wetu anao wajibu wa kushiriki katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu." Amesisitiza Waziri Ummy