Breaking

Saturday 5 March 2022

WIZARA YA AFYA KENYA YATANGAZA MLIPUKO WA HOMA YA MANJANO




Wizara ya Afya ya Kenya imetangaza mlipuko wa homa ya manjano nchini humo huku wagonjwa 15 wakiripotiwa katika kaunti ya Isiolo na kusababisha vifo vya watu watatu hadi kufikia sasa.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dk Patrick Amoth Machi 04, 2022 inasema mgonjwa wa kwanza aligunduliwa Januari 12.

Amesema kuwa hadi kufikia wakati huo jumla ya wagonjwa 15 wanaougua homa, maumivu ya misuli na viungo wameorodheshwa huku mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 11 na mkubwa zaidi ana miaka 65.

"wengi wakiwa ni vijana, wanaume huathirika zaidi,” inasomeka taarifa hiyo.

“Kwa hiyo hii ni kutoa tahadhari katika kaunti zote 47 nchini Kenya, zaidi katika kaunti zilizo hatarini kama vile Wajir, Garissa, Marsabit, Meru, Samburu, Baringo, Elgeyo Marakwet, Pokot Magharibi na Turkana.” ameongeza

Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Afya nchini Kenya imepanga kufanya chanjo katika kaunti zote zenye hatari zaidi.

Ingawa hakuna dawa maalum ya kuzuia virusi vya homa ya manjano inayojulikana, ugonjwa huo unaweza kuzuilika kupitia chanjo madhubuti ambayo ni salama na bei nafuu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages