
Watu sita wamefariki Dunia na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya gari waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne April 12, 2022 eneo la Kwamdulu ambapo gari aina ya Coastal yenye namba za usajili T833 DMH kuacha njia na kupinduka.
Kamanda Jongo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya Magunga Korogwe na majeruhi wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo.
Ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva hivyo kushindwa kukata kona na gari kutelezaa kisha kupinduka na wito Kwa watumiaji wa vyombo vya Moto barabarani kufuata sheria ili kuzuiya ajali zinazoweza kuepukika.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Dk Salma Swedi amethibitisha kupokea miili 6 na majaruhi 19 na kwamba majeruhi wawili hali zao nii mbaya na wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.