Breaking

Friday 1 April 2022

TAARIFA YA KUANDAMA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN ..BAADHI YA MAENEO DUNIANI UMEONEKANA

 

Na Samir Salum - Lango la habari


Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa mwezi unaoashiria kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umeandama Jioni ya leo Ijumaa April Mosi, 2022 Katika Nchi mbalimbali ikiwemo Saudia Arabia, Kuwait, Uingereza na UAE.


Kupitia ukurasa Rasmi wa Twitter wa Msikiti Mtukufu wa Macca Haramain umeeleza kuwa mwezi huo umeonekana katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo hivyo ikiashiria kuwa Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaanza kesho April 02, 2022.


Mwezi pia umeoneokana katika Nchi za Kuwait Na Umoja wa Falme Za Kiarabu UAE hivyo Waislam Nchini humo nao wataanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa ramadhan kesho April 02, 2022


Huko Visiwani Zanzibar taarifa kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu imeeleza kuwa Mwezi  haujaandama hivyo kesho watakamilisha Mwezi wa Shaaban 30.


Nchini Oman imetangaza kuwa mfungo wa mwezi wa Ramadan utaanza Jumapili tarehe 03 Aprili.

Sultani wa Oman umetangaza kuwa kamati ya muandamo wa mwezi wa Ramadhani imesema rasmi kuwa muandamo wa mwezi  haujathibitishwa, na kesho Jumamosi ni kukamilika kwa mwezi wa Shaaban, na Jumapili ni mwanzo wa mwezi wa Ramadhani.

Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi!



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages