Breaking

Wednesday, 13 April 2022

WATU WANNE WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA NYAYA ZA UMEME




Watu wanne Jijini Dar es Salaam wamekamatwa kwa tuhuma za kuiba nyaya za umeme na kutaka kuziuza ikiwa ni kujaribu kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro amewataja Watuhumiwa hao kuwa ni OMARY ALLY, miaka 28, Mkazi wa Tegeta na mwenzake JUMA SULLEIMAN, Miaka 30, Mrangi, mkazi wa Wazo na wanunuzi wa vifaa hivyo ni AMOS JOHN, miaka 30, mkazi wa Tegeta na MOKOLO MACHAGE, miaka 26, mkazi wa Bunju.

Kamanda Muliro amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa April 10, 2022 na baada ya kuhojiwa wamekiri kuhusika katika matukio ya namna hiyo.

Ameongeza kuwa baada ya kupekuliwa maeneo yao walikutwa na viroba vinne vya Nyaya za Copper zilizochunwa.

Aidha Kamanda Muliro ametoa onyo kali na kuwa Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma na atakayejaribu atakamatwa na mifumo ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria itazingatiwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages