Breaking

Monday 30 May 2022

MAREKANI KUSITISHA MSAADA WA NDEGE ZA KIVITA UKRAINE


Na Said Muhibu, Lango La Habari 


Nchi ya Marekani imetangaza kusitisha utoaji wa msaada wa ndege za kivita nchini Ukraine kufuatia tishio lililotolewa na Urusi kuwa kitendo hicho kitapelekea ongezeko la kuzalisha silaha nzito nchini humo pamoja na kuchochea zaidi mzozo baina ya Urusi na Ukraine.


Kauli iliyotolewa na Rais wa Marekani Joe Biden leo inafuata baada ya Urusi kutoa onyo kwa nchi za Magharibi kusitisha utoaji wa msaada wa silaha za kivita kwa Ukraine siku ya Alhamis Mei 26, 2022.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alionya mataifa ya Magharibi dhidi ya kuipatia Ukraine silaha zenye uwezo wa kushambulia eneo la Urusi, akionya kwamba hatua hiyo itakuwa hatua mbaya kuelekea ongezeko la uzalishaji wa silaha lisilokubalika nchini humo.


Maoni ya kiongozi wa Marekani Biden yalitolewa na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, yalifuatia ripoti za wiki iliyopita kwamba Washington ilikuwa inajiandaa kutuma mifumo ya juu ya ndege za kivita ya masafa marefu huko Kyiv.


Aidha, Viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana mjini Brussels kujadili pendekezo la awamu ya sita ya vikwazo dhidi ya Urusi, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya mafuta.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages