.jpeg)
Watu wasiopungua 44 wamekufa na wengine hawajulikani waliko baada ya mvua za masika zinazoendelea kunyesha kusababisha maafa kaskazini mashariki mwa nchi ya Brazil.
Waziri wa maendeleo ya majimbo Daniel Ferreira jana Jumapili Mei 29, 2022 amewaambia waandishi habari kuwa mbali ya waliopoteza maisha liko kundi la watu 56 ambao bado hawajulikani waliko, 25 waliojeruhiwa na maelfu wengine wanaoiishi bila maakazi baada ya mvua kuharibu nyumba zao.
"Tulisajili watu 44 waliofariki, 56 hawajulikani walipo, 25 waliojeruhiwa, 3,957 bila makao na 533 wamekimbia makazi yao," Ferreira aliuambia mkutano wa waandishi wa habari huko Recife, mji mkuu wa jimbo la kaskazini-mashariki la Pernambuco.
Juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari kiasi maafisa 1,200 wako kwenye jimbo la Pernambuco kusaidia kazi ya kuwatafuta waliopotea na kuwapeleka maeneo salama wale waliokwama kutokana na mvua.
Juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari kiasi maafisa 1,200 wako kwenye jimbo la Pernambuco kusaidia kazi ya kuwatafuta waliopotea na kuwapeleka maeneo salama wale waliokwama kutokana na mvua.
Idadi ya waliofariki iliongezeka kutoka 34 tangu Jumamosi, huku takriban 28 wakiuawa katika maporomoko ya ardhi, huku mvua kubwa ikinyesha na kusababisha mito kufurika na tope likisomba kila kitu kilichokuwa kwenye njia yao.
Kati ya Ijumaa usiku na Jumamosi asubuhi, kiasi cha mvua kilifikia asilimia 70 ya kile kilichotabiriwa mwezi wote wa Mei katika baadhi ya maeneo ya Recife.