Breaking

Friday 13 May 2022

ROYAL TOUR ITALETA MAENDELEO KATIKA KILA SEKTA NCHINI - DKT. ABBAS


Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamaduni,Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitangaza Tanzania kupitia Royal Tour. Dkt, Hassan Abbasi amesema filamu hiyo ni lango linalokwenda kufungua maendeleo kwenye kila sekta hapa nchini.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 13, 2022 kwenye Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali jijini Tanga Kauli mbiu ikiwa ni " Mawasiliano ya Kimkakati nyenzo muhimu kufanikisha  sensa ya Watu na Makazi 2022"


Dkt, Abbasi ametoa wito kwa Maafisa Habari kuitangaza  na amemkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali nakala ya filamu hiyo ili isambazwe nchini kupitia kwa maafisa hao.

Akitaja baadhi ya faida ya filamu hiyo amesema inakwenda kutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja katika kipindi kifupi.

Aidha, amesema katika uzinduzi uliofanywa nchini Marekani ambako ni soko kuu la utalii wa Tanzania ameweza kukutana na viongozi matajiri namba moja katika sekta mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.

Ameongeza kuwa filamu hiyo ya kihistoria,  imetengenezwa katika kiwango cha kimataifa na wataalam nguli duniani ambao pia wanamitandao mikubwa  ya kuisambaza.


Ametumia fursa hiyo kumpongeza  Mhe. Rais kwa kazi kubwa aliyofanya na kuwaomba maafisa Habari na watanzania kwa ujumla  kumwombea katika kazi kubwa anayoifanya ya kuitangaza na kufungua Tanzania duniani ili kuvuta wawekezaji na watalii nchini.

"Nampongeza Mhe. Rais kwa kushiriki moja kwa moja katika kuitengeneza filamu hii haikuwa kazi rahisi" amesisitiza Dkt. Abbasi

Kikao kazi hicho kimefungwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ambaye amesisitiza Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kusemea mafanikio ya Serikali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages