Breaking

Thursday 23 June 2022

AMUUA NDUGU YAKE KWA KUMPIGA FIMBO KICHWANI WAKIGOMBANIA MKATE



Mwananchi mmoja Mkazi wa Kabuku Wilayani Handeni Mkoani Tanga, Juma Mgetu (55) amefariki Dunia baada ya kupigwa fimbo na mwezake huku chanzo kikielezwa kuwa walikuwa wakigombea mkate.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea June 18,2022 ambapo chanzo cha tukio hilo ni marehemu na ndugu yake walikuwa wakigombania mkate ndipo Mtuhumiwa alimpiga Juma na fimbo kichwani na kupelekea kifo chake.

Aidha kutokana kuendelea kwa matukio ya uhalifu kwenye baadhi ya maeneo Kamanda Jongo amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa kuanzisha ulinzi shirikishi ili kuweza kutoa taarifa zinazohusu wahalifu kwenye maeneo yao.

Kuhusu malezi Kamanda ameendelea kutoa wito kwa Wazazi na walezi kuzingatia suala la malezi bora kwa Watoto na kuwajengea misingi ya hofu ya Mungu ili kuijenga jamii iliyo bora.


Source: Millard Ayo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages