Breaking

Friday 24 June 2022

FIFA YAIPIGA RUNGU LA ADHABU GEITA GOLD

Na Said Muhibu, Lango La Habari 


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeipa adhabu klabu ya ligi kuu Tanzania bara NBC Geita Gold kufanya usajili kwa madirisha mawili.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo June 24, 2022 imesema adhabu hiyo imekuja baada ya Geita Gold kushidwa kumlipa mishahara aliyekuwa kocha wake Etienne Ndayiragije wakati akiifundisha klabu hiyo.


Kocha huyo raia wa Burundi alipeleka madai yake FIFA akidai fidia ya kuvunjiwa mkataba pamoja na malipo mengine wakati akiifundisha timu hiyo ya mkoani Geita.


FIFA italazimika kuwasilisha suala hilo katika kamati ya nidhamu ya FIFA kwa hatua zaidi za kinidhamu iwapo Geita Gold hawatamlipa kocha huyo.


Aidha, TFF imezishauri klabu za ligi kuu Tanzania NBC kuheshimu mikataba ambayo zinazoingia na wachezaji na makocha, kwani hiyo ni moja ya vigezo vya kupata leseni za klabu Club (License Regulations)

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages