Breaking

Tuesday 14 June 2022

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KAGERA KUJA NA HATI PONGEZI KWA RAIS SAMIA

Na Lydia Lugakila, Kagera


Jumuiya ya wafanyabiashara  Mkoa wa Kagera wameazimia kutoa hati kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutokana na kusamehewa madeni ya tozo na Kodi mbali mbali.


Kauli hiyo imetolewa juni 13, 2022 na Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Kagera, Nicholaus Jovin  walipokutana na waandishi wa habari katika hoteli ya victorious iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.


Jovin amesema kuwa hatua hiyo ya furaha kwa wafanyabiashara hao imekuja kutokana na kauli ya Rais Samia aliyoitoa hivi karibuni akiwa Mkoani Kagera katika ziara ya siku 3 ambapo alitoa msamaha wa kodi iliyokuwa imelimbikizwa kwa muda mrefu.


"Sisi kama wafanyabiashara wa Mkoa huu tunaipongeza serikali ya awamu ya sita kupitia Rais Samia kwakweli kauli yake imechochea muitikio kwa wafanyabiashara kufanya shughuli zetu bila wasi wasi kwani kipindi cha nyuma tulikumbana na changamoto nyingi" alisema mwenyekiti wa jumuiya hiyo.


Aidha ameongeza kuwa   wanaahidi kushirikiana bega kwa bega na kufanya mabadiliko yatakayofanya Mkoa huo unaondokana na tatizo la kuwa nyuma kiuchumi.


Kwa upande wao wajumbe wa jumuiya hiyo akiwemo Richard Maganga wamesema kauli ya Rais hakika imewapa nguvu za kupambana kiuchumi.

Mwisho 



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages