Breaking

Thursday 2 June 2022

RAIS SAMIA AWATAKA MAKATIBU MAHSUSI KUTUNZA SIRI ZA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Makatibu Mahsusi wa Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022. 
Makatibu Mahsusi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiimba na kushangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Zawadi Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Bi. Zuhura Songambele Maganga kabla ya kufungua Mkutano huo Mkuu wa Kitaaluma kwa Makatibu hao Mahsusi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.
********

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu pamoja na maafisa Utumishi kutunza siri za Serikali.


Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa Tisa (09) wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).


Aidha, Rais Samia amesema suala la utunzaji wa siri za Serikali linasaidia kuepuka madhara yanayoweza kuwapata watu binafsi, Taasisi, Serikali na usalama wa Taifa letu.


Rais Samia pia amesema weledi, uaminifu, uadilifu na uzalendo ndiyo njia pekee itakayowafanya Makatibu Mahsusi kuaminiwa, kutegemewa na kuwawezesha kusonga mbele katika majukumu yao.


Katika hatua nyingine, Rais Samia ameridhia Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora kuwa maalum kwa ajili ya mafunzo ya uhazili kwa ngazi zote ili kuzalisha Makatibu Mahsusi ambao watakwenda kutumika katika Taasisi za Serikali.


Halikadhalika, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbalimbali ya kada za kiutumishi, na maslahi ya watumishi wa umma kwa ujumla.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages