Breaking

Wednesday 1 June 2022

RAIS SAMIA AZINDUA KITABU CHA MAISHA YA SUGU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amezindua kitabu cha mwanamuziki nguli wa Hip Hop, Mr 2 Proud au maarufu kama Sugu kiitwacho muziki na maisha kwenye tamasha la kutimiza miaka 30 katika tasnia hiyo.


Katika tamasha hilo lililoitwa  The dream  concert,  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, watendaji wa Wizara na wadau mbalimbali wamehudhuria.


Tamasha hili limepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sugu mwenyewe ambaye ametumbuiza na kukonga nyoyo za mamia ya watu waliohudhuria. 


Mhe. Rais amemtunukia tuzo, Sugu huku akimpongeza kuwa miongoni wasanii wenye nyimbo zenye maadili.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages