Breaking

Thursday 16 June 2022

TEMBO WARRIORS WAPEWA HESHIMA BUNGENI


Timu ya Taifa ya Walemavu ( Tembo Worriors) leo Juni 16,2022 imekaribishwa  katika Bunge na Dkt.Tulia Akson kwa ajili ya kupongezwa na Waheshimiwa Wabunge kufuatia mashujaa hao kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India baadae Mwaka huu.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewasilisha salamu za pongezi kwa Tembo Worriors mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Akson ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Juni 16, 2022 Dodoma.

Katika tukio hilo Waziri Mhe. Mohammed Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Viongozi wengine wa wizara na Timu hiyo wamehudhuria.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages