Breaking

Friday, 29 July 2022

MKUFUNZI WA SENSA AKUTWA AMEFARIKI GESTIBahati Msengi ambaye ni mkufunzi wa sensa amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni, Kata ya Kanyenye mkoani Tabora.

Mkufunzi huyo ambaye pia alikuwa afisa elimu kata ya Milambo, wilayani Kaliua mkoani humo, alihudhuria mafunzo ya siku 21 yaliyomalizika juzi Jumanne na kufungwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, katika Chuo Cha Ualimu Tabora.

Msengi alikutwa amefariki jana Jumatano Julai 27, 2022 saa nane mchana katika nyumba ya kulala wageni ya Wema.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo ni kifo cha kawaida kama vifo vingine vinavyotokea hospitalini.

 Soma zaidi <<HAPA>>

Source: Mwananchi

Pages