Breaking

Tuesday 12 July 2022

AJALI YAUA WATU NANE, WATANO WA FAMILIA MOJA - BIHARAMULO



Watu wanane wamefariki dunia watano wakiwa wa familia moja baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika barabara kuu ya kutoka Lusahunga kwenda Nyakahura wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Julai 12, 2022.

Amesema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mercedes Benz lililokuwa likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda, mkazi wa Nyamata Rugesela EAST Province.

Kamanda huyo amesema, gari hilo lilikuwa linakwenda jijiji Dar es Salaam liligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Succeed lililokuwa likiendeshwa na Nyawenda Bihera Bisalo (35), Muha ambaye ni mkazi wa Lusahunga.

Amesema katika ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu wanane ambao ni dreva huyo na abiria wake saba na watano walikuwa wa familia moja.

Amewataja marehemu hao ni Nyawenda Bisalo (35) na Majaliwa Maige (32), mkazi wa Kikoma.

Watano wa familia moja ni ambao ni wakazi wa Nyamalagala ni,

Jesca Ntahimula (45), Magreth Kimuna (14), Adidas Sekanabo (12), Zabloni (6) na Vedastina Sekanabo (8) mkazi wa Kikoma.

Amesema katika uchunguzi wa awali wa jeshi hilo umebaini chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dreva wa gari aliyehama kutoka upande wake wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia kitendo kilichosababisha kugongana uso kwa uso kwa magari hayo.

Kamanda huyo amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Kituo cha Afya Nyakanazi.

Amesema dreva wa lori, Vicent Gakuba alitoroka baada ya ajali hiyo ila polisi walifanikiwa kumkamata baada ya muda mfupi katika kizuizi cha Kahaza mpakani mwa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, akiwa katika Lori lililokuwa likielekea nchini Rwanda na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.


Source: Mwananchi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages