Breaking

Monday 25 July 2022

BABA WA KAMBO AMCHOMA MTOTO KWA CHUMA CHA MOTO KISA KUPOTEZA PESA YA KUNUNULIA SIGARA





Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 anauguza majeraha mabaya ya moto baada ya kuchomwa na babake wa kambo kwa kupoteza shilingi 196 (10Ksh).

Tukio hili lilipigwa ripoti kwa kituo cha polisi cha Kibaoni na wahudumu wa hospitali eneo la Muhamarani Kibaoni, Mpeketoni, Kaunti ya Lamu ambako mtoto huyo alikimbizwa kwa matibabu.

Ripoti ya polisi inaarifu kuwa mshukiwa kwa jina Samuel Mwangi, alitumia chuma kimoto kwenye mikoni, miguu na makalio ya moto huyo baada ya kumtuhumu kupoteza pesa zake ambazo zilistahili kununua sigara.

Mama wa mtoto huyo hakuwa nyumbani wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa afisa wa Shirika la Waislamu la Kutetea Haki za Binadamu (MUHURI) tawi la Kaunti ya Laumu Mohammed Skanda mshukiwa amekamatwa na atafikishwa katika Mahakama ya Mpeketoni.

“Mshukiwa amekamatwa lakini angali kusomewa mashtaka mahakamani kwa kuwa mtoto huyo badi hajaandikisha taarifa kutokana na maumivu anayopitia kwa sasa,” Skanda alisema.

Kwa mujibu wa afisa huyo, shirika lao kwa ushirikiano na maafisa wa jinsia wanafuatilia suala hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha mtoto huyo anapata haki.

“Atawafikishwa mahakamani Jumatano ili kujibu mashtaka. Tunafuatilia suala hilo kwa karibu sana ili kuhakikisha mtoto huyo anapata haki,” Skanda alisema.

Mvulana huyo yuko katika uangalizi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpeketoni ambako bado anapokea matibabu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages