Breaking

Monday 25 July 2022

MBOWE MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA VIJANA DUNIANI SHINYANGA



Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Mhe. Freeman Mbowe anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yatakayofanyika Mjini Shinyanga Agosti 12,2022.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumapili Julai 24,2022 Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Mhe. Emmanuel Ntobi amesema maandalizi ya Maadhimisho ya Siku Vijana duniani ambayo kitaifa mwaka huu yanafanyika mkoani Shinyanga yanaendelea vizuri.

Ntobi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani mkoani Shinyanga amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akiambatana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.

“Tunapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa maadhimisho ya siku ya vijana duniani iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2020 kwa mara ya kwanza nchini Tanzania inafanyika mkoani Shinyanga katika ukumbi wa Lyakare Hotel ambapo tunaratajia kupokea wageni zaidi ya 4000 kutoka ndani na nje ya nchi”,amesema Ntobi.

Amesema maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kitaifa yameandaliwa na Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) huku akibainisha kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na Bonanza la Michezo mbalimbali Agosti 11,2022 na Agosti 12,2022 kutakuwa na maonesho ya kazi za ubunifu za vijana.

“Tumejiandaa vyema kupokea wageni tunaomba pia wafanyabiashara na wajasiriamali waendelee kujiandaa kupokea vijana kutoka ndani nan je ya nchi. Wenye nyumba za kulala wageni ‘hotel, logde, guest house’, migahawa, mama lishe wajiandae kupokea wageni, hii ni fursa nzuri kwa mkoa wetu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara”,ameeleza Ntobi.


Source: Malunde 1 Blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages