Breaking

Thursday 7 July 2022

BRELA NA NIDA KUBORESHA HUDUMA


Na Mwandishi wetu- Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amesema uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) zitasaidia wananchi kupata huduma mbalimbali na wawekezaji kuwekeza kwa wingi Nchini.


Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo  Jijini Dodoma  wakati wa kikao cha Makatibu na Wakuu wa Taasisi kujadili utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA).


Amesema  kutatuliwa kwa changamoto zinazokabili mamlaka hizo kunatoa fursa kwa wafanyabiashara  kuanzisha bishara zao, viwanda kwa mujibu wa sheria hivyo kuongeza pato la mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla.

###MWISHO###

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages