Breaking

Tuesday 26 July 2022

LATRA YAPIGA MARUFUKU MAHUBIRI, MUZIKI MKUBWA, VIDEO CHAFU NDANI YA MABASI
Na Dotto Kwilasa,DODOMA

MAMLAKA ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) imepiga marufuku mahubiri , biashara ,muziki mkubwa na picha zisizo na Maadili kufanyika ndani ya vyombo vya usafiri na kudai kuwa vitu hivyo vinaleta kero kwa abiria.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo (LATRA ) Habibu Suluo amesema hayo leo Julai 26,2022 wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekekezaji wa shughuli za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekekezaji kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema kumekuwa na baadhi ya vyombo hivyo kukiuka miiko ya usafirishaji na kutoa rai kwa abiria kutoa taarifa mapema endapo gari walilopanda linaruhusu huduma hizo kuendelea ndani ya basi huku safari ikiwa inaendelea.

"Tutambue kuwa kelele inapozidi viwango huathiri afya ya mwanadamu na wanaoathirika sana ni watoto na wazee,inapaswa kujua kuwa pale unapopiga kelele kupita kiasi inapunguza umakini, kupelekea migogoro,kupunguza umakini vifo na kusababisha msongo wa mawazo,"amesema.

Pamoja na hayo amesema magari hayo ya abiria yanapokuwa na kelele husababisha abiria kukosa utulivu, kutokulala, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kupelekea shinikizo la damu, hivyo kanuni zimewekwa ili kulinda afya za binadamu na kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

"Lazima tushirikiane kuwalinda abiria,huduma hizo ndani ya mabasi ni marufuku kufanyika kwani zimekuwa zikileta hisia tofauti kwa sababu kila msafiri anaimani tofauti tofauti,"amesema

Pamoja na hayo amewataka wasafirishaji kuzingatia kanuni taratibu na miongozo ilizowekwa na Mamlaka Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) mahubiri ndani ya mabasi hayaitajiki na endapo ikabainika basi linafanya huduma hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa dereva na Mmiliki wa gari hilo.

Akiongelea juu ya baadhi ya magari kuwabagua baadhi ya abiria Johansen Kahatano Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabarani alibainisha tabia hiyo ni kosa kisheria na haivumiliki na endapo ikitokea mtu afanyiwa kitendo hicho apekeke malalamiko yake katika mamlaka husika.


Source: Malunde 1 Blog 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages