Breaking

Thursday 28 July 2022

MADIWANI TABORA WASIKITISHWA ALIYEKUWA DC KUTEULIWA KUWA RC, WAMTUMIA UJUMBE RAIS SAMIA

Dk Yahaya Nawanda Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu.

Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Tabora wamesikitishwa na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Dk Yahaya Nawanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Dk Nawanda ni miongoni mwa wakuu wa wilaya waliopandishwa kuwa wakuu wa mikoa katika mabadiliko aliyoyafanya Rais Samia usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 28, 2022.

Dk Nawanda alikuwa Tabora na sasa anakwenda kuchukua nafasi ya David Kafulila ambaye kwenye mabadiliko hayo amewekwa kando.

Akizungumza katika Baraza la Madiwani leo Alhamisi Julai 28, 2022, Meya wa Manispaa ya Tabora, Ramadhan Kapela amesema wamesikitishwa kuondoka kwa Dk Nawanda ingawa wanafurahi kupandishwa kwake kuwa mkuu wa mkoa.


"Tunasikitishwa kuondoka kwake (Dk Nawanda) kwani alikuwa anashirikiana nasi vizuri lakini tunafurahi anaenda kuwa mkuu wa mkoa," amesema

TazamaRAIS SAMIA ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA

Amesema baada ya kuondoka kwake, wanatamani Rais Samia ateue mkuu wa wilaya mwenye sifa kama za Dk Nawanda ambaye hakuwa na makuu.

Dk Nawanda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mwaka Juni 2022.

Source: Mwananchi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages