Breaking

Saturday 23 July 2022

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA KIGOMA, MWINGINE ATOWEKA



Majambazi wawili wameuawa huku Jambazi mmoja akitoweka kusikojulikana baada ya majibizano ya risasi wakati Majambazi hao walipovamia soko la kijiji cha Bukirilo lililopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.

Kaimu kamanda jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Menrad Sindano amesema Jeshi la Polisi wakishirikiana na Askari wa JWTZ usiku wa July 21,2022 Majambazi watatu walifyatua risasi hewani kuwatisha Wafanyabiashara na Wananchi kisha wakafanikiwa kuiba vitu mbalimbali ikiwemo vitenge, pesa na simu.

Kamansa Sindano amesema Askari Polisi waliokua doria na Askari wa JWTZ detach ya bukirilo walifika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwajeruhi Majambazi wawili kwa risasi ambapo walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa Hospitali huku mmoja akikimbia.

Polisi wamesema baada ya kufanya ukaguzi eneo la tukio wamekamata silaha moja aina ya AK.47 na magazine mbili, moja ikiwa na risasi 15 nyingine ikiwa tupu na pia maganda matatu ya risasi.


“Katika upekuzi wa miili ya marehemu hao zimepatikana simu 9 zilizoporwa kwenye duka na pesa Tsh.82,000 na vitambulisho vyao ambavyo vinaonyesha wanatoka nchi jirani”
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages