Breaking

Wednesday 27 July 2022

MAWAZIRI WIZARA YA MADINI WATETA NA WABUNGE UKANDA WA MADINI YA TANZANITE



Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko pamoja na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wamekutana na kuzungumza na waheshimiwa Wabunge wa Ukanda yanapochimbwa Madini ya Tanzanite ili kujadili na kutoa maoni kuhusu pendekezo la Mfumo wa uendeshaji na udhibiti wa biashara ya Madini ya Tanzanite.
Mbali na Wabunge, mkutano huo umehudhuriwa pia na watendaji kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake.

Mkutano huo umefanyika leo Julai 27, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) Mkoani Arusha.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages