Breaking

Thursday 21 July 2022

NAIBU WAZIRI MASANJA AKAGUA ENEO LILILOPANDWA MITI NA TFS MAGU, ATOA MAAGIZO



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) Jumatano Julai 20, 2022 amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Shule ya Msingi Sagani lililopandwa miti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika Machi 21, 2022 Wilayani Magu Mkoani Mwanza.

Lengo la ziara hiyo ni kuangalia maendeleo ya miti iliyopandwa na Wakala wa Huduma wa Misitu Tanzania (TFS) endapo inatunzwa vizuri au la.

Mhe. Masanja amemuagiza Mkuu wa Shule ya Msingi Sagani, Ruhumbika Kapesa, kuendelea kusimamia ukuaji wa miti hiyo ili ifikie lengo lililokusudiwa la kuifanya Wilaya ya Magu kuwa ya kijani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages