Breaking

Saturday 9 July 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI LEO JULAI 09, 2022




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Habibu Suluo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Malaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 9, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Suluo anachukua nafasi ya Gilliard Ngewe ambaye amemaliza mkataba wake.

Kabla ya uteuzi huo Suluo alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu, Shirika la Wakala na Meli za Tanzania (TASAC).

Taarifa imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages