Breaking

Friday 19 August 2022

CASEMIRO ANUKIA MANCHESTER UNITED



Na Vintan Godfrid

Kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Real Madrid Carlos Henrique Maarufu kama Casemiro anatarajiwa kujiunga na klabu ya mashetani wekundu wa Uingereza klabu ya Manchester United mwisho wa juma hili.

Klabu ya Manchester united imefikia makubaliano na klabu ya Real Madrid baada ya dau waliloweka Euro milion 60 na maongezo ya euro milion 10 kukubaliwa na pande zote klabu na na mchezaji mwenyewe.

Casemiro hakukataaa baada ya kuwasilishiwa ofa hiyo na kuulizwa na kocha wake achague kwenda Jijini Manchester kuwatumikia Red devils au abaki kuendelea na Real akaishia kuchagua ofa nzuri iliyoletwa na mashetani wekundu.

Ukamilisho wa uhamisho huo unatarajiwa kukamilika mwisho wa wiki hii ikiwa bado mambo machache yanashughulikiwa kama vile vipimo vya Afya , visa na vinginevyo.

Uamuzi wa Manchester United kumsajili Casemiro unakuja baada ya jitihada zao kumsajili kiungo wa Timu ya taifa Uholanzi na Klabu ya Barcelona Frenkie de Jong kugonga mwamba au kuwa katika sintofahamu.

Manchester United wamekuwa na wakati mbaya sana katika ligi kuu ya uingereza ilioanza hivi karibuni kwa kupoteza michezo miwili ambapo pia imechagizwa na kukosa utulivu katika eneo la kiungo mkabaji na ushambuliaji.




Source: Marca
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages