
Tazama HAPA CHINI
Wakati sensa ya Watu na Makazi ikiendelea nchini, makarani wawili wamejikuta katika wakati mgumu baada kuporwa vifaa vyao vya kukusanyia taarifa maarufu kama vishikwambi na vibaka.
Tukio la kwanza limetokea jijini Arusha ambapo karani aliyetambuliwa kwa jina la Saraphia Kiwango ameporwa kishikwambi chake alipokuwa akielekea kuanza kuhesabu makundi maalum katika Kata ya Unga Ltd jijini Arusha huku mumewe akijeruhiwa kichwani na vibaka waliokuwa kwenye bodaboda.