Breaking

Thursday 4 August 2022

WAZIRI BASHINGWA AWAPA MAAGIZO MAZITO MA-RC, MA-RAS, MA-DC NA MA-DED KUELEKEA ZOEZI LA SENSA



Na OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amewaagiza wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri nchini kutotoka kwenye maeneo yao ya kazi mpaka zoezi la sensa litakapokamilika.

Ametoa maagizo hayo leo Agosti 4, 2022 jijini Dodoma alipokuwa akielezea umuhimu wa zoezi la sensa na uhusika wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye kukamilisha zoezi hilo ambapo amesema viongozi hao watapaswa kuondoka kwenye maeneo yao kwa kibali maalum.

Amesema kuwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa inajukumu la kuhakikisha inashirikiana na Kamati ya Uratibu wa Sensa Kitaifa ili kuhakikisha zoezi la Sensa linafanikiwa kwa asilimia mia moja.

Bashungwa amefafanua kuwa kama kutatokea dharura ambayo itamlazimisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kulazimika kutoka kwenye maeneo yake ya kazi lazima kuwasilisha taarifa kwa Waziri.

Aidha, Ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia zoezi la Sensa katika Mikoa yao ili kutatua changamoto ambazo zinaweza kujitokeza kwenye zoezi hilo badala ya kusubiri kwa muda mrefu na kuleta dosari ambazo zinaweza kufanya zoezi la sense kutofanyika kwa ufanisi.

Pia, Bashungwa amewaagiza Makatibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Waheshimiwa madiwani, wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuendelea kutoa ushirikiano kikamilifu kwa viongozi ambao wanasimamiazoezi la Sensa katika maeneo yao ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia 100.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages