Breaking

Thursday 4 August 2022

MTOTO AJIUA KWA KUNYWA SUMU KISA KUFOKEWA NA BABA YAKE

Picha hauhusiani na tukio

Mtoto mmoja Wilayani Makete mkoa wa Njombe amekutwa amefariki kwa kujiua kutokana na kunywa sumu baada ya kuonywa kwa kufokewa na Baba yake aliyekuwa akimuonya baada ya kuwaacha punda waliokwenda kula mazao kwenye shamba la Watu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Mtoto huyo aliacha punda aliokuwa nao machungani na kwenda kucheza na Watoto wenzake hali iliyomfanya Baba yake kumuonya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwenye shamba.

“Huyu Mtoto alipewa punda akachunge, akawaacha na akaenda kucheza na matokeo yake wale punda wakala shamba la Mtu, Mzee wake akalalamikiwa ndipo akamuita Mtoto lakini kitendo cha Mzee kumfokea yule Mtoto achunge punda kwa umakini, yeye akachukua maamuzi magumu akatafuta sumu akanywa na kufariki”

Kamanda Issah ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutafuta njia sahihi ya kuzungumza na Watoto huku pia akiomba Makanisa na Misikiti kuendelea kutoa mafunzo mema ya dini Kwa Watoto ili kutokuwa na maamuzi magumu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages