Breaking

Thursday 4 August 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MSCL, TBC



Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi August 04, 2022 amemteua amemteua Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).


Kabla ya uteuzi huo Hamissi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).


Aidha Rais Samia amemteua Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).


Kagaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbet Mrango ambaye amemaliza kipindi chake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages