Breaking

Wednesday 10 August 2022

RC CHALAMILA ATANGAZA KIAMA KWA WATUMISHI WATAKAOKWAMISHA JUHUDI ZA SERIKALI

 


Na Lydia Lugakila, Lango la habari

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert John Chalamila ametangaza kiama kwa watumishi watakaokwamisha juhudi za serikali ikiwemo kutowajibika ipasavyo katika maeneo yao ya kazi pamoja na wabadhilifu wa mali za umma.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo Agosti 9, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa (Mayunga) uliopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

RC Chalamila amesema hayupo tayari kuvumilia watumishi wazembe wanaokwamisha maendeleo ya mkoa kwa uzembe wao.

"Wadokozi wa mali za umma waanze kuomba toba ipo pia tabia za kuzorota katika kazi nitapambana na mtumishi wa umma atakayekwamisha juhudi za serikali alisema Rc Chalamila.

Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kuzitembelea kata zote za Mkoa wa Kagera ili kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinawakabili wananchi wa Mkoa huo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages