Breaking

Saturday 13 August 2022

MAYELE AWATETEMESHA SIMBA, YANGA MABINGWA NGAO YA JAMII 2022/23


Na Said Muhibu, Lango La Habari

Klabu ya Young Africans imefanikiwa kutwaa kombe la Ngao ya Jamii dhidi ya klabu ya Simba Sports Club kwa mwaka wa msimu 2022/2023.


Mchezo uliochezwa hii leo August 13, 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam uliwakutanisha watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba na Yanga kufanikiwa kuifunga Simba mabao 2-1.


Simba ilitangulia kutikisa nyavu za Yanga kupitia Kiungo Mshambuliaji wake Pape Ousmane Sakho na kutamatika kwa kipindi cha kwanza Simba ikiwa kinara kwa bao 1-0.


Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa Klabu ya Yanga, Jesus Moloko na Bernard Morrison wakiingia kuchukua nafasi za Sure Boy na Farid Mussa. Yanga ilifanikiwa kupindua meza kupitia Mshambuliaji wake Fiston Kalala Mayele ambaye aliingia nyavuni mara mbili na kufanikiwa kuipatia Yanga ubingwa huku mchezo ukitamatika kwa Yanga kushinda magoli 2-1.


Hadi hivi sasa klabu hizo mbili zimekutana mara 105 huku Yanga ikipata ushindi mara 38 na Simba 28 na wakitoa sare mara 42.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages