Breaking

Monday 10 October 2022

RAIS SAMIA ATEUA WAKILI MKUU WA SERIKALI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Oktoba 10, 2022 amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali ambapo kabla ya uteuzi huo Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Bwana Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Aidha Rais Samia Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali ambapo kabla ya uteuzi huu Bi. Mwaipopo alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Bi Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ametuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Taarifa imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 09 Oktoba, 2022.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages