Breaking

Tuesday 22 November 2022

AKUTWA AMEFARIKI KWENYE BWAWA NJOMBE



MWANAUME mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 mpaka 35 amekutwa amefariki katika Bwawa dogo lililopo katika Msitu wa TANWAT eneo la Kibena Mjini Njombe.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni Walinzi katika Msitu ya Tanwat uliopo karibu na Bwawa hilo wamesema kuwa mnamo majira ya saa 11;10 Alfajiri ya tarehe 21 hii leo waligundua uwepo wa mtu ambaye alikuwa akisogea katika Bwawa hilo huku akiwa ameshika Tochi na baada ya kufika akaanza kuingia ndani ya Bwawa hilo na hata walipojaribu kumuita ili atoke nje ya Bwawa hakuwasikiliza.

Akizungumza na Vyombo vya Habari baada ya kuutoa mwili katika Bwawa Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Njombe, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Inspekta Joel Mwakanyasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Baada ya Mwili Huo kutolewa katika Bwawa, Jeshi la Zimamoto liliwataka wananchi kuutambua mwili huo lakini Wananchi akiwemo George Mlangwa wamekiri kutomfahamu mtu huyo.


Kufuatia tukio hilo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Njombe limewaasa Wananchi kuacha mara Moja tabia ya kusogelea maji yenye kina kirefu ikiwa hawana Uwezo wa kuogelea.

Via: Malunde 1 Blog 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages