Breaking

Tuesday 22 November 2022

MAFUNDI WANAOJENGA MAJENGO YA SERIKALI WATAKIWA KUPATIWA MAFUNZO



Na. Angela Msimbira NZEGA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa mafundi wanaopewa kazi ya kujenga majengo ya Serikali.

Mafundi hao ni wale wanaojenga majengo ya Serikali katika ngazi za Halmashauri kwa mfumo wa fource akaunti lengo likiwa ni kuwa na majengo bora na imara.

Kairuki ameyasema hayo Novemba 21, 2022 wakati akikagua ujenzi wa madarasa kwenye Shule ya Sekondari ya Kampala iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

Amesema Serikali iliona kuna umuhimu wa kuwatumia mafundi wa kawaida kwa ajili ya kupunguza gharama za ujenzi tofauti na awali ilipokuwa wakitumika wakandarasi.

Amewaagiza Wakurugenzi kuhakikisha wanatoa mafunzo kabla ya ujenzi wa majengo ya Serikali kwa lengo la kupunguza makosa ambayo huweza kujitokeza baada ya kukamilisha ujenzi

"Ili kupunguza dosari zinazoweza kujitokeza baada ya kukamilisha ujenzi ni vyema mafundi hao wakapatiwa uelewa wa namna ya kujenga majengo yenye ubora na imara" amesisitiza Waziri Kairuki
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages