Breaking

Tuesday, 29 November 2022

BABA AMNAJISI MWANAE WA MIAKA 10 HOSPITALINIPolisi katika Kaunti ya Kakamega wamemkamata mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 40 kwa tuhumza za kumnajisi binti yake mwenye umri wa miaka 10 aliyelazwa hospitalini.

Mshukiwa aliomba wauguzi katika Hospitali ya Kaundi ndogo ya Navakholo kumruhusu kwa usiku huo kuwa na mwanawe aliyekuwa amelazwa hospitalini aikugua malaria. Kisa hicho cha kusikitisha kiliripotiwa na mwanamke aliyekuwa akimlinda msichana huyo hospitalini na ambaye alishuhudia kisa hicho.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Navakholo Richard Omanga amesema kuwa polisi waliotembelea hospitali hiyo walibaini kuwa ni kweli msichana huyo alikuwa amenajisiwa.

“Baada ya kupata ripoti, maafisa wetu walienda katika hospitali hiyo kuchunguza kisa hicho na kupata kuwa ni kweli msichana huyo alikuwa amenajisiwa,” Omanga amesema.

Kwa mujibu wa Omanga, mshukiwa aliondoka hospitalini na kurejea baadaye kisha kuwapumbaza wauguzi kuwa alitaka kumlinda binti yake.

“Mwanamume huyo alienda kutafuta pesa na kurejea jioni bila pesa. Kisha akaomba kuwa na binti yake kwenye wadi kwa usiku huo hadi asubuhi - fursa ambayo alitumia kumnajisi bintiye,” Omanga alionegeza,

Mshukuwa anasemekana kutalikiana na mke wake na alikuwa akiishi na binti yake pekee yake.


Via: Tuko

Pages