Breaking

Thursday 17 November 2022

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA KAGERA




Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamefariki dunia kutokana na kupigwa risasi na polisi usiku wa kuamkia jana, baada ya kutokea majibizano ya risasi baina ya kundi la watu watano na askari, katika Kijiji cha Muganza, Kata Mursagamba wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera William Mwampaghale, amesema kuwa kuuawa kwa watu hao kumetokana na oparesheni maalumu inayofanywa na jeshi hilo katika maeneo mbalimbali ya mkoa hasa mipakani, inayolenga kudhibiti uhalifu wa kutumia silaha iliyoanza mwezi Septemba mwaka huu.

Kamanda Mwampaghale amesema kuwa wakati wakiendelea na oparesheni hiyo Novemba 15, 2022 walipata taarifa fiche kutoka kwa raia wema kuwa kuna kundi la watu wanajiandaa kufanya uhalifu kwa kutumia silaha, na kwamba ilipotimu saa 04:30 usiku waliweka mtego katika barabara itokayo Bugarama kwenda Muganza na kufanikiwa kuwaona watu hao.

"Waliamrishwa na polisi kusimama lakini walikataa na kuanza kupiga risasi, kwa kuwa kulikuwa na giza na ni usiku, polisi walijibu na kuwajeruhi watu watatu wenye jinsia ya kiume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 ambao hawajatambuliwa kwa majina, na watu hao walifariki wakati wakipelekwa hospitali ya Nyamiaga, huku wengine wawili wakikimbia" amesema RPC Kagera

Soma zaidi >>HAPA<< Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages