Breaking

Monday 28 November 2022

MAJAMBAZI WAVAMIA KANISA LA SDA KUPORA WAUMINI SIMU, PESA



Waumini wa kanisa la SDA jijini Johannesburg walipoteza vitu vya thamani ikiwemo pesa taslimu wakati wa ibada ya kanisani.

Ripoti zinaonyesha kuwa wanaume sita waliokuwa wamejihami na bunduki walivamia kanisa hilo huku mhubiri akitoa mahubiri kwenye mimbari.

Kulingana na taarifa ya uongozi wa kanisa hilo, tukio hilo lilinaswa kwenye kanda iliyokuwa ikipeperusha ibada hiyo moja kwa moja siku ya Jumamosi.

Mhubiri wa kanisa hilo ambaye kwa hakika anaonekana alikuwa na hofu iliyomvaa usoni mwake, alikwenda kuketi baada ya majambazi kumkatiza akieneza injili.

"Wapendwa washiriki wa Kanisa la Johannesburg Central SDA, Kanisa lingependa kuchukua nafasi hii kuwahakikishia kwamba hili pia, litapita. Hakuna linalodumu milele. Kama viongozi, tunaliombea kanisa kuungana katika nyakati kama hizi, tukiunga mkono kila mmoja. Mengine ya kimaadili na kimatendo tukutane kanisani kesho (Jumapili, Novemba 27), saa 10 asubuhi ibada ya ushauri inaanza. Basi tuwepo dakika chache kabla ya 10. Asante, Mungu atujalie sote amani na uhakika wa uwepo wake," taarifa hiyo ilisoma.

News24 inaripoti kuwa msemaji wa polisi wa Gauteng, Kanali Noxolo Kweza alithibitisha kisa hicho katika taarifa akisema waumini waliibiwa vitu vyao vya thamani kwa mtutu wa bunduki.

"Waliwatishia waumini wa kanisa hilo na bunduki hakuna mtu aliyejeruhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa, watuhumiwa walitoka nje ya kanisa, polisi watafanya kila jitahada kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wezi hao, ili waumini wa kanisa waruhusiwe kufanya shughuli zao kwa amani. ."

Tukio hilo linakuja wiki chache baada ya lingine sawia na hilo ambapo pasta aliuawa kwa kupigwa risasi, na waumini wengine wawili kujeruhiwa vibaya.

Kulingana na gazeti la The Citizen, watu watano waliokuwa wamejihami kwa bunduki walivamia ibada ya kanisa eneo la Diepsloot na kuanza kufyatua risasi kiholela.



Via: Tuko
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages