Breaking

Wednesday 16 November 2022

RAIS DKT. MWINYI ATEUA VIONGOZI WAWILI



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili leo Jumatano Novemba 16, 2022.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Mhandisi Zena Said imeeleza kuwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua Dk Sharifa Omar Salim kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma.

Dk Sharifa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Pia, Dk Mwinyi amemteua Dk Hashim Hamza Chande kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anaeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Kabla ya uteuzi huo, Dk Hashim alikuwa Mkuu wa Skuli ya Kilimo, Kizimbani katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages