Breaking

Monday 14 November 2022

WANANCHI TABATA KISIWANI KUPATA AHUENI HUDUMA YA MAJI KUPITIA VISIMA VIREFU



Kisima cha Tabata Kisiwani kinachomilikiwa na DAWASA chenye urefu wa mita 58 kimesafishwa na kimeingizwa katika mfumo rasmi wa maji.

Kisima hiki kipo Tabata, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam kina uwezo wa kuzalisha lita 1,440,000 kwa siku na kinatarajiwa kunufaisha wakazi wa Tabata Kisiwani, Twiga, Mandela chini, Mandela juu, Mawenzi, Kichefuchefu na baadhi ya maeneo ya Kimanga.


Matengenezo haya yanategemewa kukamilika na kuanza kutoa huduma ya usambazaji maji ndani ya wiki hii.

DAWASA imefufua visima 14 na kufanya jumla ya visima vya DAWASA kuwa 162 vinavyozalisha jumla zaidi ya lita milioni 30 kwa siku.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages